Skip to main content Skip to main navigation menu Skip to site footer
JTKF.png

Jarida la Taaluma za Kiswahili na Fasihi

Publisher: Sentam Research & Publishing

About the Journal

Jarida la Taaluma za Kiswahili na Fasihi (Limefupishwa kama JTKF) ni mojawapo ya majarida yanayo milikiwa na Kampuni ya Sentam Research and Publishing. Lengo kuu la jarida hili ni kuchangia ukuwaji wa lugha ya Kiswahili inayoenziwa na wengi haswa ukanda wa Africa Mashariki. Jarida hili litachapisha makala zote zinazolenga kukikuza Kiswahili kama vile uchambuzi wa lugha, ushairi, tamthilia na mengineyo. JTKF linataka kuwa jukwaa mashuhuri la kimataifa linaloendeleza maarifa, utamaduni na matumizi ya Kiswahili. Jarida hili linakaribisha utafiti wa kielimu unaochunguza mchango wa Kiswahili katika maendeleo ya jamii, utambulisho wa kitamaduni, na mijadala ya kijamii. JTKF linachapisha makala za utafiti, tafsiri, mapitio ya vitabu, na uchambuzi wa kazi za kifasihi.